ISHI NDANI YA NDOTO YAKO

in #life8 years ago

Akiwa na miaka 5 Alifiwa na Baba yake,

Akiwa na miaka 16 aliamua kuacha shule,

Akiwa na miaka 17 tayari alikua kapoteza ajira 4,

Akiwa na miaka 18 aliamua kuoa,

Akiwa na miaka kati ya 18-22, alikua msimazi wa njia za reli lakini alishindwa akafukuzwa,

Baadae alijiunga na Jeshi lakini akafukuzwa pia,

Akatuma maombi shule ya sheria ila hakupata nafasi,

Akawa muuzaji wa Bima lakini alishindwa pia,

Akiwa na miaka 19, alifanikiwa kuwa Baba,

Akiwa na miaka 20, Mke aliamua kuondoka na mtoto,

Hatimaye akapata ajira kama mpishi na mwosha vyombo wa mgahawa mdogo,

Alishindwa hata katika jaribio la kumpata mwanae, na kuamua kumshawishi mkewe kurejea nyumbani,

Akiwa na miaka 65 alistaafu ajira yake ya kupika na kuosha vyombo katika mgahawa,

Baada ya kustaafu alipata mafao yake kutoka serikalini dola 105 $, kama Tsh 231,000/=.

Alidhani serikali imemuona kama hajiwezi kabisa,

Akafanya jaribio la kujiua, akiamini hakuna thamani ya kuishi tena, na kwamba ameshashindwa sana. Hakufanikiwa hata ktk jaribio lake hilo,

Akaamua kukaa chini ya mti na kuandika matarajio yake, Ila aliona ayaandike yale aliyoyakamilisha tayari,

Akagundua kuna mambo mengi hakuyafanya bado. Akagundua lipo jambo moja ambalo anaweza kulifanya vizuri zaidi kuliko mtu yeyote yule anayemfahamu,

Na Ilikua ni namna gani ya Kupika,

Akaamua kuchukua dola 87 $ kama Tsh 191,400/= kutoka kwenye Hundi yake ya pensheni na kununua kuku. Akawakaanga kwa kuwachanganya na viungo anuai akapata mchanganyiko wa aina yake (unaovutia),

Akaamua kupita mlango kwa mlango kuwauza kwa majirani zake huko Kentucky. Mchanganyiko ule ukapendwa sana na akaamua kuanzisha mgahawa wake uitwao Kentucky Fried Chicken (KFC) uliokua ukitengeneza mchanganyiko wa kuku alioubuni.

Hatimaye biashara yake ikakua na akafungua migahawa mingi ya KFC nchini Marekani. Mchanganyiko ule ukazidi kupendwa na kutanua wigo wa biashara yake.

Huyu si mwingine ni Colonel Harland Sanders mwanzilishi wa migahawa ya KFC duniani. Licha ya kustaafu akiwa "fukara wa kutupwa" katika umri wa miaka 65, lakini hadi wakati anafariki (1980) akiwa na umri wa miaka 90 alikua katika orodha ya mabilionea wakubwa nchini Marekani.

Kwa sasa migahawa ya KFC imeenea kote duniani katika nchi 123, Tanzania ikiwemo, na ni mgahawa wa pili mkubwa ulioenea zaidi duniani baada ya migahawa ya McDonald's.

Mwaka 2013 migahawa ya KFC ulifanya mauzo ya dola Bilioni 23 sawa na Tsh Trilioni 50. Maana yake ni kwamba mauzo ya KFC kwa mwaka mmoja ni sawa na bajeti ya Tanzania kwa miaka miwili.

Kumbuka muasisi alikua FUKARA hadi uzee wake (miaka 65) na akadhani ameshindwa maisha. Akajaribu kujiua. Lakini baada ya kutafakari akaona bado ana nafasi ya kujaribu tena. Akajaribu japo katika umri wa uzee, na hatimaye Mungu akamfanikisha. Akawa BILIONEA MKUBWA sana nchini Marekani.

Je wewe umekata tamaa ya maisha? Ulitamani kusoma lakini ukashindwa kwa kukosa ada? Umesoma lakini umekosa ajira? Miaka inapita na unaona wenzio wanaajiriwa wewe uko tu nyumbani? Je Umejaribu biashara lakini kila wakati unapata tu hasara? Unahisi kukata tamaa? Unahisi Mungu amekuacha?

Usikate tamaa. Mungu hajakuacha. Jipange tena na uanze upya. Haujakawia bado.... Kitu kikubwa ni "Mtazamo" ( Attitude).

Usikate tamaa .... Haijalishi mambo ni magumu kiasi gani. Una kila kitu cha kukufanya Ufanikiwe, Amua kubadili mtazamo ili kubadili Stori ya maisha yako. Inawezekana, anza sasa.! .............